Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa,
baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi
30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika
ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za
wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika
mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi
mkoani Rukwa
Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri
bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri, mkuatno huo wa Namanyere
Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
Mzee
Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali
kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa
bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa
ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka
2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la
Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika.
Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na
waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali
katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani
Nkasi. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment