Timu
ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini kesho
(Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi
dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Intamba
Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi
na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa
10 jioni.
Nayo
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye
hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi
kutoka Kenya.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na
kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh.
10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
MALINZI
AWAPONGEZA SUKER, LEKJAA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza
marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuongoza
mashirikisho ya mpira wa miguu katika nchi zao.
Suker
amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia (CFF)
wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco
(FRFM).
Katika
salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amesema ushindi waliopata ni uthibitisho
kuwa familia ya mpira wa miguu katika nchi zao ina imani kubwa kwao katika
kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi hizo.
Rais
Malinzi amesema Lekjaa na Suker wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ambayo
tayari imefanyika, lakini vilevile kuja na mawazo mapya ambayo yatakuwa
changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini Morocco na Croatia kwa ujumla.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment