Timu ya Taifa
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la
Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo
wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de
Janeiro, Brazil.
Hadi
mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika
mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za
mwisho.
Kwa
matokeo hayo, Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa
leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga
Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.
Mchezo huo
wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati
ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George
Osborne.
Katika
mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi
na kutoka sare ya mabao 2-2.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment