Moshi
WATUMIWA SUGU WA KUCHAKACHUA
VIROBA VYA KONYAGI WASHINDWA DHAMANA NA KURUDISHWA RUMANDE.
WAELEZEWA NI WATU HATARI SANA
WAIOFAA KUACHILIWA KWA DHAMAN
WANATUHUMA KILA PEMBE YA NCHI IKIWEMO DAR ES SALAAM
YAELEZWA, KONYAGI FEKI WANAZOTENGENEZA ZIMEATHIRI WATANZANIA WENGI
BAADHI YA WAMILIKI WA MABAA
WALIOHUDHURIA MAHAKAMANI HAPO WAMETOA RAI KWA WANANCHI KUACHA KUNUNUA KONYAGI
VICHOCHORONI NA BADALA YAKE KWENYE MABAA HALALI AU MADUKANI
MAHAKAMA ya hakimu mkazi
Moshi, leo
imefurika mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia watuhumiwa sugu wa
utengenezaji wa konyagi feki na bidhaa nyingine mbalimbali na
kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa kudhuru maelfu ya watanzania.
Hata hivyo mahakama ya mkazi
moshi imewaachia kwa dhamana watuhumiwa hao nane ambao wanakabiliwa na tuhuma
za kutumia alama za biashara za makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.na kujipatia pesa kinyume cha utaratibu.
Watuhumiwa hao ni Yusuph George,
Richard Leonard, Preygod Urassa, Mohamed Rashid, Greyson Jonathan, George
Kisivani, Hagai Nelson na Jackson Shayo, ambao wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi kinyume cha sheria
huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya halali ya kampuni ya
Tanzania Distilleries Limited.
Watuhumiwa hawa wana kesi
mbalimbali ikiwemo ile ya kutumia nyaraka za mamlaka ya mapato nchini TRA
ikiwemo mihuri yenye namba za kodi ya mapato jambo ambalo linadaiwa kuikosesha
serikali mapato mengi.
Wakili wa serikali Julius Semali
ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa watuhumiwa hao ni hatari na kwamba
wanakabiliwa na kesi za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini.
Singida wana kesi ya namna hii na
ambayo itaendelea tena Aprili 30, 2014,
Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka za TRA wakati Arusha
wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.
Pamoja na kupewa dhamana kwenye
kesi hiyo huko Moshi, bado hakimu aliamuru warudishwe rumande kwa kushindwa
kutimiza masharti ya dhamana.
No comments:
Post a Comment