Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kutoka juu ya tanki,
wakati akikagua mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, leo Mei 11,
2014, alipokuwa akiendelea na ziara yake ya siku kumi katika mkoa wa
Tabora, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za
wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa juu ya tanki hilo la
mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, leo Mei 11, 2014, akiambatana
na Kinana katika ziara ya siku kumi katika mkoa wa Tabora, kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na
kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja
wa Mamlaka ya Maji safi katika Halmashauri ya Nzega, Samweli Buyigi
(kushoto), kuhusu bwawa la chanzo cha maji kilichopo katika halmashauri
hiyo ambalo limekauka kutokana na kuota magugu maji. Watatu kushoto ni
Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
Kinana
akikagua chujio la maji la Mamlaka ya Majisafi Nzega mkoani Tabora,
Pamoja naye ni Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala, na anayempa maelezo
ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Nzega, Samweli Buyigi Mkurugenzi
(kushoto)
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akijadili jambo na Kigwangala wakati akikagua
miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi mji wa Nzega, leo Mei 11, 2014.
Mbunge
wa Viti Maalum Munde Tambwe (kushoto) akimsaidia kutia mchanga kwenye
mashine ya kufyatulia mafotali, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana aliyekuwa
akishiriki kufyatua matofali ya mradi wa Jumuia ya Wanawake Tanzania
(UWT) wilaya ya Nzega, leo Mei 11, 2014. Kushoto ni Kigwangala
Mjunbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM, Hussein Bashe, akitaja mchango wake wa fedha
taslim sh. 500,000 na ahadi ya kiasi hicho hicho cha fedha kuchangia
mradi wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT wilaya ya Nzega mkoani
Tabora ambao umezinduliwa na Kinana (kulia), leo Mei 11. 2014. Wapili
kulia ni Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Mbunge wa Bukene wilayani
Nzega, Suleiman Zedi ambaye pia alichangia mradi huo sh. 500,000.
Katibu
Mkuu wa CCM Kinana na wakati Mbunge wa Nzega, Kigwangala wakitangaza
kutoa mchango wa sh. 500,000, wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa
ufyatuaji matofali wa UWT Nzega
Bashe na Kigwangala wakimwaga kicheko wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT
Jengo
la kisasa la soko jipya la Kata ya Itobo, Nzega ambalo limejengwa na
serikali hili karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kulikagua leo Mei
11, 2014
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa
hadhara aliofanya leo Mei 11, 2014 katika kijiji cha Itobo wilayani
Nzega
Wananchi wa Itobo wakimsikiliza kwa makini Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo Mei 11, 2014
Katibu Mkuu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akihutubia kwenye mkutano huo wa Itobo
Wanachama wa zamani na wapya wa CCM wakilakiapo cha utii wa CCM wakati wanachama wapya zaidi ya 85 walipokabidhiwa kadi za CCM
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akitazama bwawa ambalo hutumiwa na mwananchi wa
kijiji cha Bukene, katika kilimo cha mpunga cha umwagiliaji
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika
Uwanja wa Taifa wa Bukene, wilayani Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara
leo Mei 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake wilayani Nzega kabla ya kuanza
kesho ziara katika wilaya ya Uyui. Picha zote na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment