Kutokana
na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa
Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili
Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.
Baada
ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za
kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF
inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na
taratibu katika utendaji wao.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment