JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA
HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya
Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex
: 41051
DAR ES SALAAM, 24 Juni, 2014
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo
vya Habari
Makao Makuu ya Jeshi yanatoa taarifa kwa vyombo vya
habari kuwa, Kongamano kubwa la Kijeshi (Land Forces East Africa 2014)
litafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 14 hadi 16 Julai 2014 katika
ukumbi wa Mlimani City. Kongamano hilo ambalo litakuwa sehemu ya maadhimisho ya
miaka 50 toka kuanzishwa kwa JWTZ, litahusisha maonesho ya zana za kijeshi
yakayofanywa na makampuni zaidi ya 32 toka mataifa mbalimbali ya ndani na nje
ya Afrika.
Maonesho hayo yatatoa fursa kwa washiriki toka kada
mbalimbali kubadilishana mawazo, kuona
na kutangaza biashara ya zana mbalimbali za kijeshi. Aidha, Majeshi yatakutana
kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto za sasa za ulinzi na usalama wa
Dunia hasa eneo la Afrika Mashariki ambalo linakabiliwa na changamoto
mbalimbali ukiwemo uvuvi haramu, uharamia na jinsi ya kulinda maliasili za
Taifa.
Washiriki mbalimbali watapata fursa ya kutoa
mihadhara wakiwamo Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi toka nchi mbalimbali, mabalozi na
wawakilishi wa Jumuiya za Kimataifa.
Ili kutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo muhimu na
kubwa kuwahi kufanyika nchini, Mkuu wa Kamandi ya Nchi Kavu Meja Jenerali Salim
Kijuu atafanya mkutano na waandishi wa habari kesho tarehe 25 Juni 2014 Makao Makuu ya Jeshi Upanga saa tatu na nusu
asubuhi.
Nyote mnakaribishwa.
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0754 -
270136
No comments:
Post a Comment