Na Magreth Kinabo-
MAELEZO
Baraza la Vyama vya Siasa nchini limeamua mazungumzo ya maridhiano
kati ya pande zinazokizana kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba kutokana na mvutano ya kutaka serikali mbili au tatu yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa.
Aidha baraza hilo,limeamua kufanyike kongamano Agosti 9 na
10 mwaka huu mjini Dodoma kwa ajili ya kuangalia maslahi mapana ya taifa.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Kuga Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya
viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi
kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.
Alisema katika mkutano huo,
baraza hilo limepokea ripoti ya mkutano wa Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini na baadhi viongozi wa vyama vya siasa,
pia limepokea ripoti ya chama kimoja kimoja, ambavyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) Chama cha NCCR – MAGEUZI na Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Aidha Mziray amesema kwamba
katika mkutano huo, kuna mambo ambayo wamekubaliana na mengine hawakuafikiana.
“Baraza limeamua mazungumzo
ya mariadhiano yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa ,ambazo zitakuwa na
wajumbe wachache. Baraza linawashauri wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba
warudi Bungeni kwa kuwa ndio mahali
pekee pa kutoa hoja na wala si sehemu nyingine,” alisema Mziray.
Aliongeza kuwa
anavipongeza vyama hivyo kwa kuonesha nia ya kuendelea kwa mazungumzo hayo na wameonesha imani na baraza hilo, ambapo
wametaka majadiliano kupitia kamati
yafanyike.
Mwenyekiti huyo
akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika,
viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na
viongozi wa dini zote.
“Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na
mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano katika suala hili. Tunategemea busara za
viongozi hawa zitatubadilkisha na
kutuweka pamoja kwa maslahi ya taifa na
kuachana na mambo ya kivyama,” alisisitiza.
Aliyataja mambo ambayo, wamekubaliana kuwa yasiwepo wakati
wa kuendelea kwa Bunge hilo ni kutumia lugha za matusi na kejeli.
Katika mazungumzo
hayo, “Baraza limeona si rahisi kufikia muafaka kwani kila upande ulionesha kuwa Bunge hilo halina mamlaka ya
kubadilisha Rasimu ya Katiba Mpya, na
mwingine unadai Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha na kuboresha rasimu hiyo
kwa vile suala hilo lipo kisheria
kulingana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kifungu cha 25 na kanuni zinaruhusu,”
alisema Mziray.
Kwa upande mwingine Mziray
alisema kuwa jambo lingine lilionesha ugumu ni mvutano uliopo wa kuhusu
wa kuwepo kwa Serikali mbili au tatu kwa sababu ni suala la kisera za vyama na sera haibadilishwi
mpaka mkutano mkuu wa chama.
KWA MAWASIALIANO ZAIDI
No comments:
Post a Comment