Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvyeka miti wakati wa
uzinduzi wa kambi ya Umoja wa Vijana wa CCM, ya mafunzo ya kilimo katika
eneo la Boko Timiza, Kibaha mjini mkoa wa Pwani. Katika kambi hiyo
vijana wanatarajiwa kufanya mafunzo ya kilimo kwenye shamba la ekari 25.
Kijana akihamasisha vijana wenzake, walioko kwenye kambi hiyo ya mafunzo ya kilimo, eneo la Boko Timiza wilaya ya Kibaha mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani. |
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye kiwanja
unakofanyika ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani,
baada ya kuzindua ujenzi huo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM
wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye na Kushoto ni Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry
Koka.
Kinana
akipata burudani ya Ngonjera kutoka kwa vijana Chipukizi baada ya
kuzindua ujenzi Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mjini leo. Wapili kulia ni
Nape.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfurahia Chipukizi wa CCM, Suma
Iddi, aliyekuwepo wakati akizindua ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya ya Kibaha
mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua tangi la maji alipokagua
ujenzi wa mradi wa maji katika kitongoji cha Muheza, wilaya ya Kibaha
mkoa wa Pwani.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Tumbi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani akimpatia
maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuhusu wodi ya wagonjwa mahututi
iliyopo kwa sasa kwenye hospitali hiyo, ambapo alisema bado inahitajika
kuwepo dawa za kutosha kuliko ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment