Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai
iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama Salma ameambatana na
mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili nchini China kwa ziara ya kiserikali.
Rais Dkt.
Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing
mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa
China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), wakisikiliza kwa makini
maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bwana Wang Yilin
kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko
Beijing nchini China. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti
wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo.
Rais Dkt.
Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana
Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi
baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko
Beijing.
Rais Dkt.
Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia
vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la
CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini
wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li
Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika
kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo
katika wilaya ya Songzhuang nchini China.
Rais Dkt.
Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa
zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa
za Afrika huko Songzhuang.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada
ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais
Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji
hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada
ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais
Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji
hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha sanaa za Afrika
mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu yake.
Waanzilishi
wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong
wakimkabidhi zawadi ya picha Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya
ufunguzi rasmi wa kijiji hicho. (PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment