Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Oktoba 6 mwaka huu)
kujiwinda kwa mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini kwenye hoteli ya
Accomondia jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 26 walioitwa na
Kocha Mart Nooij kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.
Kwa
mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi
kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni
kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na
mengine kwenye uwanja mwingine.
Wachezaji
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al Markhiya
ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).
Naye
mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini
keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.
MKUTANO WA
WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari
kesho (Oktoba 6 mwaka huu). Mkutano
huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Jengo la PPF Tower.
MAFUNZO YA
USAJILI LIGI DARAJA LA PILI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha mafunzo ya usajili kwa klabu za
Ligi Daraja la Pili (SDL) yatakayofanyika kesho na keshokutwa (Oktoba 6 na 7
mwaka huu) kwenye hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia
saa 3 asubuhi.
Mafunzo
hayo yatahusu usajili wa mtandao ambao ndiyo klabu hizo zitautumia kwa ajili ya
Ligi hiyo itakayoanza baadaye mwezi ujao katika makundi manne ya timu sita sita
kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Kesho
mafunzo hayo yatakuwa kwa ajili ya maofisa wa usajili wa klabu za Abajalo,
Arusha FC, Kiluvya United, Magereza Iringa, Milambo SC, Mji Mkuu (CDA), Mkamba
Rangers, Mshikamano, Mvuvumwa FC, Navy, Njombe Mji, Singida United, Transit
Camp, Volcano FC na Wenda FC.
Oktoba
7 mwaka huu mafunzo hayo yatahusisha maofisa usajili wa klabu za Bulyanhulu FC,
Eleven Stars, JKT Rwamkoma, Kariakoo Lindi, Mbao FC, Mpanda United, Pamba, Town
Small Boys na Ujenzi Rukwa.
MABADILIKO YA
MECHI ZA FDL KUNDI B
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko kwa baadhi ya mechi za kundi
B Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kupokea barua kutoka Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) ikieleza kuwa Uwanja wa CCM Kirumba utatumika kwa
shughuli za kidini kuanzia Oktoba 16 hadi 19 mwaka huu.
Kutokana
na hali hiyo, mechi namba 17 kati ya Toto Africans na Green Warriors iliyokuwa
ichezwe kwenye uwanja huo Oktoba 18 mwaka huu sasa itafanyika Oktoba 20 mwaka
huu.
Mabadiliko
hayo pia yameathiri mechi namba 19 kati ya Green Warriors na Oljoro JKT ambayo
sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Oktoba 23 mwaka huu badala ya
Oktoba 21 mwaka huu.
Vilevile
mechi namba 25 kati ya Burkina Faso na Oljoro JKT imesogezwa mbele kwa siku
moja kutoka Oktoba 25 mwaka huu hadi Oktoba 26 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
BONIFACE
WAMBURA
MKURUGENZI
WA MASHINDANO
SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment