Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
wamekutana mwishoni mwa wiki na kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha
maendeleo ya mchezo huo nchini.
Mkutano
huo uliofanyika Dar es Salaam uliongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na kuhudhuriwa
na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na wanyeviti wa klabu za VPL.
Masuala
yaliyozungumzwa ni leseni za klabu (club licensing), maboresho ya Taifa Stars,
Kanuni za Ligi Kuu, Kombe la FA (Shirikisho) na mchango wa klabu hizo katika kuendeleza
mpira wa miguu kwa vijana.
Uwasilishaji
katika mkutano huo kuhusu maboresho ya Taifa Stars ulifanywa na Kocha Mkuu wa
timu hiyo Mart Nooij wakati leseni kwa klabu ulifanywa na Mkurugenzi wa
Mashindano wa TFF, Boniface Wambura.
Kuhusu
Kombe la FA, klabu zilifahamishwa kuwa mazungumzo kati ya TFF na mdhamini
yanaendelea, ambapo zilikaribisha wazo hilo kwa vile michuano hiyo itatoa fursa
kwa timu zao kucheza mechi nyingi za mashindano, hivyo kutoa nafasi ya kucheza
kwa wachezaji wengi zaidi.
Bingwa
wa michuano ya FA ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe
la Shirikisho barani Afrika.
Rais
Malinzi aliziomba klabu kukutana na kuwasilisha mapendekezo yao ya jinsi ya
kuchangia/kuboresha maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana, kuboresha Kanuni za
Ligi Kuu na kuboresha Kanuni za Bodi ya Ligi ili yaweze kufanyiwa kazi.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment