Mtakwimu
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo
kuhusu athari, madhara na ya
matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
Baadhi ya
wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali.
Waziri wa
Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua maadhimisho
ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika jijini Dar es salaam” na
kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria
kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Mwakilishi
kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango
wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya Taifa lolote wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.
Msanii
Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa matumizi
ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu
Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini.
Waziri wa
Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne kutoka kulia
mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu mara baada ya kufungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.
Mkurugenzi
wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya
takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika.(Picha na Aron Msigwa)
Na. Aron Msigwa –
MAELEZO.
Dar es
salaam.
SERIKALI kupitia Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea kuwapatia wananchi takwimu sahihi zinazohusu
sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na
masuala mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee wakati akifungua rasmi maadhimisho ya
Siku ya Takwimu Afrika yanaoongozwa na kauli mbiu isemayo Takwimu Huria kwa
uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Amesema upatikanaji wa
taarifa na takwimu sahihi kwa wananchi
unaongeza ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathmini
utendaji wa Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi.
Amesema Ofisi ya Taifa
ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu mbalimbali zinapatikana kwa
urahisi kupitia mtandao, machapisho na mifumo rahisi ili kuwawezesha wananchi
na wadau mbalimbali kuzipata pindi wanapozihitaji.
“ Maadhimisho ya Siku
ya Takwimu Afrika mwaka huu yanaongozwa na kauli Mbiu isemayo Takwimu Huria kwa
uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote ambayo inalenga kurahisisha
upatikanaji wa takwimu sahihi kwa urahisi na kumwezesha mtumiaji kuzipata bila
kizuizi chochote” Amesema.
Amefafanua kuwa upatikanaji wa takwimu huria
unawawezesha wananchi kujua sababu zinazoifanya serikali kutekeleza maamuzi
mbalimbali, kuongeza uwajibikaji na kuwawezesha kupima matokeo ya sera za Serikali,
kutathimini matumizi ya Serikali na kushiriki katika midahalo mbalimbali ya
kitaifa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda
Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo amesema kuwa
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yameweka msisitizo katika
kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau kupata takwimu sahihi kwa wakati.
Amesema maadhimisho
hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika kuweka msukumo wa
kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi na wadau mbalimbali wa
maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza uwazi wa utendaji wa shughuli za
serikali serikali.
Naye mwakilishi kutoka
nchi washirika wa maendeleo Bw.Jacques Morisset akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo ameeleza kuwa takwimu sahihi ni ufunguo wa maendeleo kwa nchi
yoyote duniani.
Amesema kuwa upatikanaji
wa taarifa mbalimbali unawawezesha wananchi kutambua na kupima kiwango cha
maendeleo ya nchi yao katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila
siku yakiwemo ya matumizi ya rasilimali, Elimu, ukuaji wa uchumi, shughuli za
kilimo na sekta ya viwanda na Biashara.
No comments:
Post a Comment