KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Tuesday, November 11, 2014

WAMILIKI WA BLOGS WACHAGUANA

Mwandishi wa BBC nchini Aboubakar  Famau kulia akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa mtandao huu wa matukiodaima Bw  Francis Godwin mara baada ya  kuteuliwa  kuwa makamu mwenyekiti wa wamiliki wa Blogs Tanzania 
Mtangazaji wa TBC Shaban Kisu wa pili  kulia akifuatilia  warsha ya TCRA na  Wamiliki wa Blogs nchini 
Baadhi ya  washiriki wa warsha   ya TCRA 
Baadhi  ya  wamiliki wa Blogs nchini wakiwa katika warsha  hiyo leo 
Wanahabari  na  wamiliki wa Blogs nchini  wakifuatilia warsha  hiyo 
Mkurugenzi  mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma  akifungua  warsha  hiyo  leo 

................................................................................................
MWANDISHI  wa gazeti la Jamboleo kutoka mkoani Iringa Bw Francis Godwin ameteuliwa kuwa makamu mwenyekiti  wa chama  cha   wamiliki  mitandao ya  kijamii (Blogs )Tanzania .

Godwin  ambae ni mmiliki  wa Blogs  hii ya  matukiodaima na Francisgodwinblog  ameteuliwa katika nafasi hiyo kama mwakilishi  wa  wamiliki  wote wa blogs za  mikoani  huku Joachimu  Mushi  akiteuliwa  kuwa mwenyekiti  wa  chama   hicho .













Uteuzi   huo umefanyika leo  katika ukumbi wa Mlimani City    baada ya  kumalizaka kwa warsha ya siku  moja  iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) 







Wengine   walioteuliwa nia pamoja na katibu  wa  chama   hicho Khadija  Kalili, wajumbe ni   Mdimu Henry , Wiliam Malecela,Othuman Maulid na Shamim Mwasha.

Akizungumza  mara  baada ya  uteuzi huo mwenyekiti wa chama  hicho Bw Mushi  alisema  kuwa  lengo  ni  kuhakikisha  katiba ya chama hicho inakamilika mapema  zaidi  ili chama  hicho  kiweze  kusajiliwa rasmi  .

 mkurugenzi  mkuu  wa TCRA Profesa  John Nkoma   alisema  kuwa  mamlaka  yake  itasaidia  kufanikisha  mchakato mzima  wa wamiliki  wote wa  Blogs nchini  kuwa na chama  chao na  kuwa  lengo ni  kuwawezesha  kufanya maamuzi  yao kwa  umoja na kuweza  kusimamiana wenyewe .

Profesa Nkoma  alisema  kuwa iwapo  wamiliki wa Blogs  nchini  wataanzisha  chama  chao  upo  uwezekano mkubwa  wa TCRA  kuwasaidia mchakato  huo na pia kuendelea  kuungana na chama  hicho  kwa kuendelea  kutoa elimu  zaidi.

Mbali ya  kuwataka  kuanzisha  chama  hicho  bado  aliwataka  wamiliki  wa blogs  nchini  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo kwa  kuheshimu misingi ya maadili badala ya  kutumia  vyombo  hivyo  kuvuruga maadili .
Akielezea  kuhusu uwajibikaji wa  blogs nchini kuelekea  uchaguzi mkuu wa  mwaka 2015 alitaka   kuhakikisha  wanatoa nafasi  sawa  kwa vyama  na  wagombea  wote  bila  upendeleo.

Kwa  upande wake  mkurugenzi wa idara ya habari (Maelezo ) Assah Mwambene  aliwataka  wanahabari  nchini  na  walimiki wa  Blogs  kuendelea  kuutumia  vema  Uhuru  wa  vyombo  vya  habari na kuangalia  mambo ya msingi kwa jamii badala ya  kugeuza  mitandao hiyo kuvuruga amani ya nchi.

No comments: