Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uwekaji saini wa Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga na Katibu wa Benki, John Rugambo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto) Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia).
Baadhi ya maofisa wa CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO),
Shikunzi John akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka wa benki hiyo na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John (wa pili kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
(wa pili kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya
Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi wa benki hiyo na TUICO jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei
(kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya
Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi kati ya Chama hicho na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB na
imetiliana saini mkataba na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda,
Huduma na Biashara (TUICO) wa kuboresha hali bora za wafanyakazi wa benki hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema
mafanikio yoyote ya kibiashara hayapatikani kama wafanyakazi ambao ndio
wazalishaji hwatakuwa na mazingira yenye maslahi bora na motisha mbalimbali.
Dk. Kimei
alisema nia ya CRDB ni kuboresha mahusiano kati ya mwajiri na wafanyakazi,
kuboresha mazingiraya utendaji kazi ili kuchochea ufanisi, kurasimisha
mahusiano kati ya benki na wafanyakazi kwa kuweka miongozo itakayosaidia
kupunguza mifarakano kati ya CRDB na wafanyakazi.
“Mkataba huu ni
wa miaka mitatu, utasaidia kuajiri na uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, kushughulikia
migogoro ya kikazi, uhamisho wa viongozi wa chama cha wafanyakazi sehemu ya
kazi,utaratibu wa likizo ya uzazi, likizo ya ugonjwa, ulipwaji gharama ya
usafirishaji mizigo kwa wafanyakazi wanaohamishwa, mazishi ya wazazi wa
wafanyakazi, bima na utoaji tuzo,”alisema.
No comments:
Post a Comment