Mkurugenzi
msaidizi kutoka Kamati za Bunge, Athuman Hussein akifafanua jambo wakati wa
semina ya Maalum kwa Wabunge wa Bunge la Vijana kabla ya kuanza kwa Bunge hilo.
Afisa
wa Bunge,Patson Sobha akielezea baadhi ya taratibu za kibunge wakati wa
semina kwa Wabunge wa Bunge la Vijana kabla ya kuanza kwa Bunge hilo.
Mshauri
Msaidizi wa Maswala ya Sheria wa Bunge,Matamus Fungo akifafanua namna
Muswada wa Sheria unavyopitia katika hatua mbalimbali Bungeni.
Washiriki
wa Bunge la Vijana wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa maafisa wa Bunge
kabla ya kuanza vikao vya Bunge hilo.
Washiriki wa Bunge la Vijana
wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa maafisa wa Bunge kabla ya kuanza
vikao vya Bunge hilo.
Spika wa Bunge la Vijana,Edgar Israel kutoka chuo cha St. John cha Dodoma
akiingia Bungeni tayari kwa kuanza kwa Bunge hilo.
Mpambe
wa Bunge akiweka siwa mezani tayari kwa kuanza vikao vya Bunge la Vijana.
Spika wa Bunge la Vijana,Edgar
Israel kutoka chuo cha St. John cha Dodoma akisoma dua kabla ya kuanza kwa
Bunge hilo mjini Dodoma. Waliosimama mbele yake ni Makatibu Mezani.
Spika wa Bunge la Vijana Ndg. Edgar
Israel akimuapisha aliyechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo Mussa
Yusufu kutoka chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kushika nyadhifa hiyo Bungeni
jana.
Kiongozi wa kambi ya Upinzani katika
Bunge la Vijana,Alpha Mazengo akiuliza swali kwa Spika wa Bunge hilo
wakati Bunge hilo lilipoketi katika vikao vyake jana.
Kiongozi
wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Vijana,Zacharia Magige
kutoka chuo kikuu cha Mzumbe akiwashukuru wabunge wenzie baada ya jina
lake kuthibitishwa rasmi na Bunge hilo kuwa Waziri Mkuu katika Bunge la Vijana
jana.
Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Vijana,Zacharia Magige
kutoka chuo kikuu cha Mzumbe akiwashukuru wabunge wenzie baada ya jina
lake kuthibitishwa rasmi na Bunge hilo kuwa Waziri Mkuu katika Bunge la Vijana.
Washiriki
wa Bunge la Vijana wakifuatilia Mijadala ya Bunge hilo kwa Makini.
Washiriki
wa Bunge la Vijana wakifuatilia Mijadala ya Bunge hilo kwa Makini.
Washiriki wa Bunge la Vijana
wakifuatilia Mijadala ya Bunge hilo kwa Makini.(Picha na Owen Mwandumbya-Dodoma)
Na.
Owen Mwandumbya- Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeandaa Bunge la Vijana linalofanyika
Mjini Dodoma kwa siku tatu, ikiwa ni jitihada la kuwajengea uwezo vijana wa
vyuo vikuu nchini. Bunge hilo liloanza vikao vyake juzi linalojumuisha Vijana
kutoka Vyuo Vikuu 15 vya hapa Nchini vinavyozunguka mkoa wa Dodoma.
Bunge
hilo linalotarajiwa kumalizika tarehe 3 Desemba, 2014, ni sehemu ya Mpango wa
Elimu kwa Umma ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kupitia mradi
wake wa kuwezesha uwezo wa wabunge na watumishi unaofadhiliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), umelenga kuwajenga vijana kushiriki
masuala ya kibunge kwa vitendo.
Jumla
wa wanafunzi 120 kutoka vyuo vya UDOM CBE, MIPANGO, TIA, MZUMBE St. John, VETA,
Theophili kisanji - Mbeya, MKAWA, RUAHA, chuo cha kiislam Morogoro,
Tumaini, na Chuo cha Sayansi Mbeya wamechaguliwa kuwa wabunge wa Bunge hilo.
No comments:
Post a Comment