Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando mara baada ya
kuwasili kwenye viwanja wa Shule ya Msingi Rahaleo iliyoko Manispaa ya Lindi
Mjini kwa ajili ya kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kupitia taasisi
yake kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya
Lindi Mjini.
Baadhi ya
wanafunzi wanaosoma Madarasa ya Awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo wakiwa
pamoja na walimu wao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpokea Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete wakati anawasili shuleni hapo.
Sampuli za
madawati yaliyotolewa na Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi
Mjini.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi kabla
ya kukabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi yake kwenye shule za
Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini kwenye
sherehe fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Rahaleo.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za madawati
yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift
Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali katika Manispaa ya
Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Rahaleo.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za madawati
yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift
Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali katika Manispaa ya
Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Rahaleo.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma darasa la awali
katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama Salma kukabidhi sampuli za
madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa ya Lindi Mjini.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa
Lindi, wanafunzi wa madarasa ya awali wanaosoma katika Shule ya Msingi Rahaleo
na walimu wao wakati wa sherehe ya kukabidhi sampuli za madawati.
(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment