Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer)
inatarajiwa kuodoka siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa
ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa
soka la ufukweni utakaofanyika siku ya jumapili.
Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano
dhidi ya Misri utakaofanyika siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa
fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli
kufuatia kupoteza mchezo wake awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam
mwishoni mwa wiki.
Msafara wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la
ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri
Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja
Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.
Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus
Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima,
Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby
Abdallah.
TWIGA STARS
KUWAFUATA ZAMBIA IJUMAA
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake
(Twiga Stars), unatarajiwa kuondoka nchini siku ya ijumaa kuelekea nchini
Zambia kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya
Zambia siku ya jumapili.
Twiga Stars inaanzia hatua ya pili katika kuwania kufuzu kwa
Fainali za Afrika kwa Wanawake baada ya kuwa katika nafasi za juu kwa viwango
barani Afrika, na endapo itafanikiwa kuwaondoa Wazambia itafuzu moja kwa moja
kwa fainali hizo.
Msafara utaongozwa na Blassy Kiondo (Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji), Beatrice Mgaya (kiongozi msaidizi), Rogasin Kaijage (kocha mkuu),
Nasra Juma (kocha msaidizi), Furaha Francis (Meneja), Christine Luambano
(Daktari) na Mwanahamis Abdallah (Mtunza vifaa).
Wachezaji watakokweda Zambia ni Asha Rashid, Mwajuma
Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi Minja, Amina Bilal, Fatuma Bashiri, Esther
Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna Kaimu, Najiat Abbas, Stumai Abdalla, Fauma
Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan, Fatuma Omary, Sophia Mwasikili, Fatuma
Khatibu na Etoe Mlenzi.
VPL
KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom
inatarajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa viwanja vitatu kutimua vumbi, Uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam Young Aricans watawakaribisha Kagera Sugar mchezo
utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Jijini Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa
Simba SC katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya
wenyeji Mbeya City watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani
Shinyanga kwenye uwanja wa Sokoine.
YANGA,
PLATINUM ZAINGIZA MIL 91
Mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young
Africas dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam iliingiza mil 91,660,000
kutokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh.
13,982,033, Gharama ya tiketi sh. 12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92,
Gharama za mchezo 15% sh. 9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh.
3,264,898.31 na Young Africans 60% sh.39.178,779.66
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment