Mke wa Rais
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi
Mjini Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu
Mahiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi
kuanza ziara ya kikazi ya siku 5 kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia
ya wana CCM na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kata ya Mikumbi katika Manispaa ya Lindi.
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kadi
kutoka kwa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kata ya Tulieni Mjini
Lindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) Ndugu Shaibu Rajabu Matola (Kikaptura)
aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa
mkutano mkubwa uliofanyika kwenye Kata ya Mikumbi.
Mjumbe wa
NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM
Ndugu Shaibu Rajabu Matola mara baada ya kujiunga na chama hicho. Ndugu Matola
ni miongoni mwa vijana 200 waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa
kadi katika mkutano huo.
Mjumbe
wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwahutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye Kata ya Mikumbi.
Mjumbe
wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwahutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye Kata ya Mikumbi.
Taswira mbalimbali za mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kata ya Mikumbi, Manispaa ya Lindi na kuhutubiwa na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa
Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Mama Salma Kikwete akikabidhi bati 100 na vifaa vya
bendi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Angaza iliyoko katika Manispaa ya Lindi. Anayepokea kwa niaba ya shule hiyo ni Mkuu wa Shule Mwalimu
Upendo Muro (wa tano kutoka kulia) akiwa pamoja na Ndugu Ashimun Mzava, Afisa
Elimu Sekondar, Manispaa Lindi wa nne kutoka kulia) na baadhi ya wanafunzi wa
shule hiyo. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bwana Abdallah Ulega.(PICHA NA JOHN LUKUWI)
No comments:
Post a Comment