Timu ya Taifa
ya Tanzania (Taifa Stars) leo asubuhi imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa
kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) mchezo utakaochezwa kesho
jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Tiketi za
mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja
wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na
sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum.
Taifa Stars
inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi
Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago
hivyo.
Akiongea na
waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza,
kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika
hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho.
Mayanga
amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa
siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari
na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka
ushindi.
Aidha Mayanga
amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya
kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana
kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
Tayari waamuzi
na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini
Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda),
mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba Martin Saanya kutoka Morogoro huku na
Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment