Rais wa Shrikisho
la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais
Boubacar Diara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) kwa kutwaa
Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17.
Katika salam zake
mh. Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya
utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka la Vijana.
Kwa kutwaa Ubingwa
wa vijana Afrika U17, Mali wamepata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika
kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile pamoja na nchi za Afrika Kusini,Guinea
na Nigeria.
Mali wametwaa
Ubingwa wa vijana Afrika U17 baada ya kuifunga timu ya taifa ya vijana ya
Afrika Kusini (Amajimbo's) kwa mabao 2-0.
Kwa niaba ya familia
ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania
wanawapa pongezi Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini Mali (FMF) wa kutwaa Ubingwa huo.
Aidha Rais Malizi
pia ametuma salam za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
Afrika Kusini (SAFA) Bw. Dany Jordaan kwa timu ya Amajimbo's kushika nafasi ya
pili.
Amajimbo's ndio
timu pekee kusini mwa Bara la Afrika watakaowaklisha kwenye fainali za U17 za
Dunia nchini Chile.
BEACH SOCCER YAENDELEA KUJIFUA BAMBA
BEACH
Timu ya Taifa ya
Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer) iliyoingia kambini mwishoni mwa
wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya
timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri mwishoni wiki ijayo.
Maandalizi ya
mchezo dhidi ya timu ya Misri yanaendelea vizuri Bamba Beach Kigamboni chini ya
kocha mkuu John Mwansasu ambaye aliingia kambini mwishoni mwa wiki na wachezaji
14.
Mchezo wa kwanza
unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini
Dar es salaam na marudio yake kufanyika baada
ya wiki moja nchini Misri.
Tanzania
ilifanikiwa kufuzu hatu ya pili baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya kwa
jumla ya mabao 12- 9, mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda kwa mabao 5-3,
na mchezo wa marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na ushindi wa
mabao 7-6.
Fainali za Mataifa
Afrika kwa Sola la Ufukweni (Beach Soccer) zinatarajiwa kufanyika mwezi April
2015 katika Visiwa vya Shelisheli.
VPL KUENDELEA JUMATANO
Ligi Kuu ya Vodacom
inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi katika viwanja vitatu tofauti siku ya
jumatano, Mkoani Morogoro katika uwanja wa Manungu-Turiani timu ya Mtibwa Sugar
watawaribisha majirani zao timu ya Polisi Morogoro.
Katika uwanja wa
Azam Complex - Chamazi maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha maafande wenzao
timu ya Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya, huku timu ya Ruvu Shooting wakiwa
katika Uwanja wa nyumbani Mabatini - Mlandizi kuwakaribisha timu ya Ndanda FC.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment