KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, April 17, 2015

WATU 20 WAMEKUFA KATIKA AJALI YA HIACE MKOANI MBEYA.

 Ajali imetokea mapema leo Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya ambapo Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukuia kwenye Mto Kiwira mapema  na watu 20  wamepoteza Maisha.
 Maiti zikiwa zimetolewa eneo la ajali mtoni.
Hapa ndipo gari hilo lilipo acha njia na kutumbukia mtoni. 

Kwa Ufupi
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.

Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.

Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.

No comments: