TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Taarifa
inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya
Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha
kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika kikao
hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala
mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi
yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi
kuhusu;
1.
Maandalizi
ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
2.
Taarifa
ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na
chama, kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
3.
Taarifa
za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
4.
Taarifa
ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4
vinavyounda UKAWA.
5.
Taarifa
za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la
kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015
na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara a Habari na
Mawasiliano- CHADEMA
No comments:
Post a Comment