KIKOSI CHA AZAM FC.
KIKOSI CHA YANGA SC
Hatua
ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame
Cup 2015) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa
kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Mechi
hiyo ya pili inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta
nikuvute kufuatia timu hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na
upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.
Kocha
mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi
ya Yanga, vijana wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na
ana imani wataibuka na ushindi.
Stewart
ameongeza kuwa ana wigo mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza
kushinda michezo yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa
haujaruhusu bao hata moja kuingia wavuni kwake.
Kwa
upande wa Yanga, kocha Hans Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam,
na katika mchezo wa kesho hana cha kupoteza, kikosi chake kimemalilika kila
idara kuelekea katika hatua ya robo fainali.
Hans
anajivunia kikosi chake ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo
wake wa awali iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia
katika hatua ya makundi.
Mchezo
wa kwanza wa robo fainali utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al
Shandy ya Sudan, mechi itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar
es aalaam.
Wakati
huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kesho kati ya Azam
FC dhidi ya Yanga SC.
RAIS WA FFB KUWASILI LEO
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundu (FFB), Reverien Ndikuriyo
anatarajiwa kuwasili leo saa 5 usiku jijini Dar es salaam kwa shirika la Ndege
la Rwanda Air.
Ndikuriyo
anatarjaiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamali Malinzi kisha atashuhudia
michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam
ikiwa katika hatua ya robo fainali kwa sasa.
Aidha
Vicent Nzamwita Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rwanda (FERWAFA)
anatarajiwa kuwasili nchini alhamis akiambatana na kocha wa timu ya Taifa ya
Rwanda (Amavubi) John McKinstry.
Rais
wa FERWAFA anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na
baadae kuhudhuria michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini Tanzania.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment