Mhadhiri Muandamizi kutoka Idara ya uchumi kilimo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) Morogoro, Dk. Khamaldin Mutabazi (pichani) wakati wa mahojiano na mwandishi wa mtandao wa modewjiblog.com (hayupo pichani) kwenye viunga vya kumbi za mikutano, Makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa wakati wa mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Tafiti nyingi nchi za Afrika zinahitaji uwekezaji mkubwa kufikia malengo yake ya kukabiliana na hali ya utayari wa mabadiliko ya tabianchi hii ni pamoja na kuandaa mikakati thabiti itakayoinufaisha watu wake.
Amesema hayo katika mahojiano maalum na mtandao huu mjini hapa, Mhadhiri Muandamizi kutoka Idara ya uchumi kilimo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) Morogoro, Dk. Khamaldin Mutabazi, anayeshiriki mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’ uliofanyika makao makuu ya UNESCO mjini Paris Ufaransa. Mkutano huo mkubwa duniani uliwajumuisha wanasayansi zaidi ya 2500 kutoka pembe zote duniani.
Katika mkutano huo, Dk. Mutabazi aliwasilisha mada maalum kuhusiana na utafiti waliofanya kwa wakulima wadogo wadogo namna watakavyo athirika na mabadiliko ya tabianchi hapo baadae endapo hawatachukua hatua madhubuti. Dkt Mutabazi amewapa change moto wakulima wadogo endapo wataendelea kulima kwa kutumia kilimo na teknolojia zilizopo sasa hapo baadae mabadiliko ya tabianchi yataweza kuwaathiri kwa kiwango kikubwa.
“Utafiti huu unaonesha ni jinsi gani jamii ya wakulima wadogo wadogo wanahitaji mipango thabiti ya kukabiliana na hali ya tabianchi.” amebainisha Dk. Mutabuzi. “Lakini kukiwepo na mipango ya maendeleo na jinsi ya kujimudu kwa teknolojia mbalimbali kama matumizi ya mbolea na vilevile kusimamia vizuri mashamba hii inaweza kupunguza tatizo hilo kwa wakulima hao wa kiwango cha chini”
Anasema utafiti huo, umefanyika katika bonde maji (Water basin) Wami Ruvu linalohusisha mikoa ya Morogoro, Dodoma, Pwani na Tanga, hata hivyo utafiti huo umefanywa katika mikoa ya Morogoro inayowakilisha mkoa wenye majimaji na mvua ya kutosha na ule wa Dodoma mkoa wenye ardhi kavu.
Dk. Mutabuzi anasema athari zinazoweza kuwakuta wakulima hao kama wataendelea kulima kama wanavyolima, bila kuboresha katika jinsi wanavyolima athari zitakuwa kubwa na umasikini katika jamii utaongezeka. Pia amedokezea suala la kipato kitapungua huku akielekeza kuwepo mipango mathubuti ya maendeleo. Kulingana na Dk Mutabuzi serikali inafanya kila iwezalo kupunguza kwa kiasi fulani ikiwemo suala la maendeleo katika kilimo, matumizi ya mbolea na kusimamia mazao kwenye mashamba.
Pamoja na hayo anasema kupitia mkutano huo wa wanasayansi, utasaidia Wanasayansi kujua dunia inaelekea wapi ikiwemo bara la Afrika licha ya kuwa na changamoto kubwa na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo, anasema mada nyingi zinazowakilishwa zinatoka katika mabara ya Ulaya, Asia na Amerika huku za Afrika zikiwa zinawakilishwa kwa kiwango cha chini kabisa hali ambayo hakikizi matakwa wanayoyakusudia.
Aliendelea mbele na kufafanua kwamba, tafiti nyigi za kutoka Afrika zinazofanywa na waafrika wenyewe zinakuwa ni za kuanzia chini huku tafiti nyingi za hali ya juu na kiwango kikubwa zinahitaji wawekezaji na Afrika bado haijawekeza katika ajenda zake zenyewe kukabiliana na hali hiyo.
Mhadhiri Muandamizi kutoka Idara ya uchumi kilimo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) Morogoro, Dk. Khamaldin Mutabazi (kushoto) akiwa katika mahojiano hayo na Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale, jijini Paris wakati wa mkutano huo wa wanasayansi..
No comments:
Post a Comment