Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa
mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
itakayofanyika Julai 25, 2015 Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam.
Akizungumza mara baada ya
kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini Dar es
salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema
maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na
kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa
Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Amesema
Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa
na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha, amesema
kutakuwa na Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za asili na
maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua kutoka kwa
viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini.
Bw.
Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja
zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi
watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio
yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa
zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
Ameongeza
kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo
Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha
usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu
changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji
wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR
jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Manispaa za
jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo mbalimbali
yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi ya vituo
hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.
Akizungumzia
baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji
wa waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema
kuwa Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.
Amewaagiza
Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia
hatua watumishi hao wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na
vurugu zinazoweza kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji
wananchi inatakiwa kuanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa
tarehe zilizopangwa.
Kuhusu taarifa za uwepo
wa baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji wasiohusika kusimamia
zoezi hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji hao kuacha mara moja
tabia hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na kwamba hatua kali za
kisheria zitachuliwa dhidi yao.
Pia amevitaka
Vyama vya siasa kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au kuvaa mavazi
yanayoashiria kampeni za siasa ili kuepusha vurugu.
No comments:
Post a Comment