Meneja wa Vifaa vya Huawei, Peter Zhang Nchini (kulia), akionesha aina ya simu ya Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa simu hizo. Kushoto ni Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga.
Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa ya uzinduzi huo. |
Na Dotto Mwaibale.
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo na ile ya kutengeneza simu za mkononi ya Huawei, wameshirikiana kuzindua simu mpya mbili za kisasa kwa ajili ya watumiaji wa simu za hali ya chini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Vifaa vya Huawei, Peter Zhang alizijata simu hizo ni Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja mbalimbali.
Alisema simu hizo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo mwananchi yeyote atakuwa na uwezo wa kununua kwa ajili ya kwenda na kasi ya teknolojia ya digitali.
Kwa upande wa Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga alisema wanaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania ili wote waweze kuwa kwenye digitali na kwa kuzindua simu hizo itasaidia jamii kuingia kwenye ulimwengu huo.
Alisema wateja wanaotumia mtandao wao watakaponunua simu hizo watapata ofa mbalimbali zitakazowasaidia kuendelea kupata huduma zikiwemo vifurushi na kusikiliza muziki bure kwa miezi sita.
No comments:
Post a Comment