Ofisa Mauzo, Juliana Mbogo na Ofisa Udhibiti Ubora, Betia Kaema wakiandaa dawa za kumpatia mgonjwa aliyefika katika banda la MSD.Na Mwandishi Wetu
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kufika banda la Bohari ya Dawa (MSD),
katika maonyesho ya Nanenane ili kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na MSD hapa
nchini.
Mwito huo umetolewa na Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda
ya Dodoma, John Kisembi wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma
kwenye maonyesho hayo ambayo kilele chake ni Agosti 8, mwaka huu.
Kisembi alisema kila mwaka MSD imekuwa ikishiriki katika maonesho
hayo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali
yanayoihusu MSD.
Alisema mwaka huu MSD imeshiriki katika maonesho hayo ambayo
yapo kikanda mkoani Dodoma ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanaelimishwa
kuhusu mambo mbalimbali ya kimafanikio yaliyofikiwa na MSD na yale yanayoweza
kuongezea uwanda wao wa kibiashara hivyo kuongea mauzo yao.
Alitaja mambo yaliyozingatiwa katika maonesho hayo kuwa ni
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kote nchini, upanuzi wa maghala hivyo
kuongeza uwezo wa kuhifadhi dawa kwa wingi pamoja na usambazaji dawa na vifaa
tiba kwa kutumia mfumo wa Direct Delivery (DD)
Mambo mengine ni matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA (Epicor
9), Uwekaji wa nembo ya GOT katika
vidonge, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ilikutofautisha dawa za
serikali na za binafsi, uanzishaji wa
maduka ya dawa ya jumla karibu na wananchi (MSD 24hours Community
Outlets) , pamoja kutoa elimu, sehemu maalumu ya kutolea dawa ambapo wagonjwa
wanaopatiwa vipimo katika banda la Hospitali ya Mkoa wanakuja kupatiwa dawa
katika banda la MSD.
|
No comments:
Post a Comment