Kipa
wa timu ya soka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akichupa kuzuia
mpira wa penati bila mafanikio wakati timu hiyo ilipomenyana na ile ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wakati
wa bonanza la pamoja la taasisi hizo mbili lililoandaliwa na PPF na kufanyika
kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam
leo Septemba 5, 2015. Katika bonanza hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, zawadi
mbalimbali zilitolewa kwa washindi wa michezo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku,
mbio za magunia, soka na mpira wa wavu. (Volleyball)
NA
K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wamefanya bonanza
la michezo kwenye uwanja wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam, leo Septemba 5, 2015 ili kuonyesha ushirikiano.
Akizungumza
kwenye bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa
PPF, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, amesema, bonanza hilo
limewakutanisha pamoja wafanyakazi wa taasisi hizo mbili za umma, ili kuonyesha
mshikamano na ushirikiano sio tu katika Nyanja ya kazi bali pia katika Nyanja
ya michezo na burudani.
Bonanza
hilo lilishirikisha michezo ya kuvuta kamba, soka, mpira wa wafu (Volleyball),
mbio za magunia, na kufukuza kuku, ambapo washindi walijinyakulia zawadi
mbalimbali. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Mazoezi ya viongo kwa wote
Mkurugenzi
wa Uwekezaji, Mfuko wa Pensheni wa PPF, Steven Alfred, (mbele kushoto),
akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, akioungana na wafanyakazi wa PPF na
wale wa NHIF kwenye mazoezi ya viungo
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, hakuwa nyuma kuwaongoza wafanyakazi wenzake kwenye mazoezi ya viungo
Mbio za kuku
Mbio za Magunia
Mpira wa wavu, (Basketball)
Mpira wa soka, kati ya PPF, na NHIF
Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari kuelezea lengo la Bonanza hilo
Timu ya soka ya PPF
Hotuba kutoka kwa Afisa wa PPF
Hotuba ya Afisa Masoko na Elimu kwa Umma, wa NHIF, Sabina Komba
No comments:
Post a Comment