KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, October 6, 2016

DC NDEJEMBI ASHIRIKI ZOEZI LA KUVURUGA BUSTANI ZILIZOLIMWA KARIBU NA VICHOTEO VYA MAJI.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akishiriki katika zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi.




Na Mathias Canal, Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi ameshiriki katika zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

Dc Ndejembi ameamua kufanya zoezi hilo la kuharibu bustani hizo baada ya wananchi Karibu na vyanzo hivyo vya maji baada ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo kuamua kulima bustani za mboga mboga kwa kutumia maji ya bomba ambayo hupaswa kusukumwa kujaza tanki la kutunzia maji.

Uharibifu huo umefanywa na Dc Ndejembi huku akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kongwa ikiwa ni sehemu ya utendaji Kazi na kuhamasisha ufanisi wa ukuzaji wa kilimo chenye tija.

Dc Ndejembi ameamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa wananchi hao wamekuwa wakifungulia maji ya bomba na hatimaye kumwagika chini ili kumwagilia bustani zao nyakati za usiku muda ambao pampu inasukuma maji kuelekea kwenye Tanki lililopo makao makuu ya Wilaya ambalo hujazwa ili maji hayo yaweze kuwahudumia wakazi wa Mjini Kongwa.

Kadhia hiyo ya kufunguliwa maji kwa kificho nyakati za usiku imesababisha kutojaa kwa Tanki hilo Hali ambayo imesababisha kukosekana kwa maji katika maeneo ya Wilaya ya Kongwa.

Kabla ya kuanza kwa zoezi hilo la kuvuruga bustani hizo Dc Ndejembi aliamuru wananchi waliohudhuria katika zoezi hilo kuchuma mboga mboga zilizokuwepo katika bustani hizo sambamba na kuchota maji yote ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika bustani hizo kwa ajili ya kumwagilia bustani hizo.

Vichoteo vilivyotobolewa katika bomba kuu ambalo linalekea Mjini vipo katika kijiji cha Ibwaga ambavyo vilianzishwa maalumu kwa ajili ya kusaidia wanakijiji wa vijiji vya karibu

No comments: