KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, October 29, 2016

KANALI NDAGALA AWATAKA WAKULIMA WA KAKONKO KULIMA MAZAO YAO KITAALAM NA KUHIFADHI CHAKULA.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani humo wakati wa ziara yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akilima moja ya shamba la mkulima.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaomba wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika kitaalamu zaidi na kujiunga kwenye vyama vya ushirika.

Ndagala pia amewataka wakulima hao kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.

Akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto katengera jana wakati wa ziara yake , vijiji vya Kinonko,Nyamibuye na Rumashi,  Ndagala alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuuza mazao yote na kupelekea kubaki wakilia njaa baada ya mazao yao waliyo lima kuisha ,pia wakulima wanatakiwa kuunda vikindi vya ushirika vitakavyo wasaidia kupata mikopo,pembejeo na masoko yatakayo wasaidia kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.

Alisema Wakulima wakiweza kulima misimu yote miwili ya Kiangazi na masika bonde hilo linauwezo wa kuhidumia wananchi wote wa Kakonko kutokana na mkulima mmoja katika hekali moja anauwezo wa kuzalisha gunia tatu za mpunga kwa msimu mmoja wa mavuno na hali inayo weza kuikomboa wilaya hiyo isikumbwe na janga la njaa.

Aidha Ndagala amewaomba maafisa kilimo wa Wilaya hiyo kuwawezesha wakulima kulima kwa misimu miwili na kuwapa mbinu za kulima kitaalamu kwa kutumia pembejeo zinazotolewa na Serikali ilikuweza kupata Mazao mengi na  kuweka tahadhali kutokana na hali ya hewa inayo weza kupelekea ukosefu wa mvua.

"Niwaombe wananchi kwa mwaka huu mlime mazao yanayo weza kustahimili ukame kama Vile mihogo, mtama na viazi na yale yanayo stawi haraka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi yaliyojitokeza hali inaweza kusababisha mwaka huu chakula kika kosekana kabisa pia mjenge tabia ya kuhifadhi chakula msikiuze chote tusije tukaanza kuomba misaada wakati uwezo wa kuhifadhi chakula tynao",alisema Ndagala.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Muhdin Alfani alisema  bonde hilo lina zaidi ya kilomita 29 na linawakulima 310 na mradi wa kukamilisha ujenzi wa bonde hilo la umwagiliaji ni shilingi milioni 312 na kila hekari moja inazalisha gunia 18 kwa msimu mmoja wa kilimo.

Alisema lengo la Halmashauri kuanzisha mradi huo ni kuwasaidia wananchi wa Wilaya hiyo kulima na kupata mazao ya kutosha yatakayo wasaidia kuilisha wilaya na Nchi jirani ya Burundi ambayo inategemea chakula kingi kutoka kwa Watanzania katika masoko ya ujirani mwema na kuweza kuiongezea serikali pato la taifa.

Nao baadhi ya wakulima wa bonde hilo,Issa Masumo na Shedrack Milembe  wameiomba Halmashauri hiyo kuwawezesha kupata masoko na kupangiwa bei maalumu itakayo wasaidia kuepukana na unyanyasaji wa Wafanya biashara wanaokuja kununua mpunga na kuwapunja wakulima na kukosa haki yao ya msingi wao kama wakulima.

No comments: