Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama Cha kikomunisti cha China (CPC) Ndugu Liu Yunshan, mjini Chongqing, nchini China hivi karibuni. Katika Mazungumzo hayo, Ndugu Kinana aliwawakilisha Makatibu Wakuu kutoka vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao alifuatana nao nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akiwa katika kikao na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe).
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akishikana mikono kuonyesha mshikamano na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe). PICHA ZOTE NA OFISI YA KATIBU MKUU WA CCM.
No comments:
Post a Comment