KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Tuesday, December 20, 2016

MAWAZIRI WAPONGEZA PPF,NSSF KWA KUUNGANISHA NGUVU KUWEKEZA KWENYE KIWANDA KIKUBWA CHA MIWA MKOANI MOROGORO



Waziri huyo alihimiza taasisi hizo kufanya haraka kukamilisha upembuzi yakinifu, ili utekelezaji kamili wa mradi ufanyike.

Dk Mpango aliwataka wahandisi kuhakikisha wanatoka maofisini ili kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana na mradi huo ikiwemo barabara inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kuelekea eneo la mradi  “Ile barabara ndio itatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali  kutoka na kuelekea kiwandani ni vyema kusimamia kikamilifu” alisema Dk, Mpango huku akikisisitiza Kampuni ya SUMA JKT kutekeleza mradi huo kwa kiwango cha ubora ili kulinda imani ya Serikali kwa makampuni ya umma katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali.

Waziri Dk. Mpango pia aliwapongeza wanakijiji kwa kuupokea mradi kwa ari ya hali ya juu, na kwamba serikali itahakikisha suala la fidia linakamilika kwa haraka ili kuepusha mivutano wakati tayari mradi umekwishakamilika.

Awali Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, akizungumza wakati wa mkutano huo aliwashukuru NSSF na PPF kwa kuleta mradi huo katika mkoa wa Morogoro ambapo mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa huduma za kijamii ambapo Dk Kebwe aliwataka vijana wa eneo hilo kufanya kazi na kuchangamkia mradi unaokuja badala ya kuwategemea wanawake na wazee katika shughuli za uzajishaji.



Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, akihutubia wanakijiji wa kijiji cha Kidunda, Kata ya Mkulazi, Tarafa ya Ngerengere mkoani Morogoro wakati wa ziara yake na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama.(wakwanza kulia). Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mkulazi Holding, Ca


No comments: