Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza kabla ya kutoa ahadi alizoahidi wakati wa zira ya kutembelea Wilaya za Mkoa wake.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ,akimkabidhi hundi ya Sh.13,000,000 Meya wa Ilala.
Akimkabidhi fedha sh.1,000,000,muuza Vitunguu Soko la Temeke Sterio, Evans Mhagama
Akimkabidhi Sh.200,00 Muuza Supu awali akiuza Machungwa,Zuhura Waziri.
Waathilika wa Madawa ya Kulevya Sober House wakipokea TV na vifaa vyake.
Akikabidhi Tumba Afisa habari Makao Makuu ya Jeshi Kombaini ya Bendi,Hope Stanley Dagaa.
Akimkabidhi Pikipiki Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni,Baluh Mwakilanga (kushoto) na Mkewe.
Akizungumza na waandishi wa habari
Akimkabidhi funguo za gari Kamanda wa FFU Kanda Maalum ya Dar es Salaam,ACP Stanley Kulyamo.
ACP Stanley Kulyamo. akijaribu gari.
Akiwakabidhi mabati
Akimkabidhi Mkuu wa shule ya Katoliki Mifuko 1,000 ya saruji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atekeleza ahadi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda
alifanya ziara katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe
19/11/2016 hadi 28/11/2016. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa alitoa
ahadi mbalimbali kwa jamii, taasisi na watu binafsi. Ahadi hizo zililenga kutoa
majawabu kwa kero zilizotolewa na wahusika.
Leo tarehe 14/12/2016 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam anatimiza ahadi zake kwa kukabidhi vifaa mbalimbali kwa
walioahidiwa. Vifaa vinavyokabidhiwa leo vina thamani ya Sh. 164,272,000/=.
Mchanganuo wa ahadi hizo na wahusika ni kama
ifuatavyo:
1.
Sober House – kuwaunga mkono juhudi zao za
kuwahudumia waathirika wa madawa ya kulevya:
Ø Jiko la Gesi (540,000/=).
Ø Mitungi 2 ya gesi (240,000/=).
Ø King’amuzi (150,000/=).
Ø Television 49’’ (1,750,000/=).
Ø Magodoro 50 (1,250,000/=).
Jumla ndogo 3,930,000/=
2.
Kutokana na utendaji wao uliotukuka Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa zawadi ya pikipiki ili
kuwapa morali ya kazi wafuatao:
Ø Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni pikipiki 1 (1,500,000/=).
Ø Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni pikipiki
1 (1,500,000/=).
Ø Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa zawadi kwa
watumishi 4 ambao utendaji kazi wao umedhihirisha hali yao ya utayari wa
kujitolea na kufanya kazi kwa ufanisi wa hali yajuu. Watumishi hao wamezawadiwa
kulala siku 1 katika Hoteli ya Hyatt the Kilimanjaro kwa gharama ya shilingi 5,232,000/= nao ni:
Ø Dr. Grace Magembe – Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam
Ø Kamishna Mruto – Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke
Ø Edward Otieno – Katibu Tawala Msaidizi Uchumi
na Uzalishaji, Sekretarieti ya Mkoa
Ø Aron Joseph – Mkurugenzi wa Uendeshaji,
DAWASCO
3.
Kuunga mkono ujasiriamali:
Ø Kijana wa Soko la Temeke Sterio kupatiwa fedha
ili kuimarisha mtaji wake (1,000,000/=).
Ø Mama muuza machungwa amepatiwa kiasi cha
shilingi 200,000= ili kuimalisha mtaji wake wa biashara
4.
Kuongeza upatikanaji wa maji:
Ø Kutokana na changamoto ya maji katika Jimbo
la Ukonga unaotokana na ubovu wa miundombinu ya kusambazia maji na kufanya
kukosekana kwa maji kwa muda mrefu, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa na kumkabidhi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala cheki ya shilingi 13,000,000/= ili wananchi wa Gongo la Mboto na Pugu waweze kupata
maji.
Ø Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa shilingi 500,000/= ikiwa ni mchango kwa ajili ya
kukamilisha ununuzi wa tanki la maji kwa wananchi wa Buyuni, Kata ya Pemba
Mnazi
5.
Kuunga mkono ujenzi na ukarabati:
Ø Jitegemee Sekondari kupewa mabati 2,000 (36,000,000/=).
Ø Shule ya Msingi Mbagala Annex kupewa mabati 1,000 (18,000,000/=).
Ø Shule ya Katoliki kupewa mifuko 1,000 ya saruji (11,000,000/=).
Ø Kutoa matofali 10,000 kwa ajili ya kanisa la
AIC (11,000,000/=)
Ø Soko la Samaki Msasani kupewa mabati 300 (5,100,000/=).
Ø Kutoa mabati 200 kwa ajili ya Uwanja wa Taifa (3,600,000/=)
6.
Kuimarisha vikundi vya sanaa (Vifaa vya
muziki ):
Ø Kukabidhi Tumba kwa kwaya ya JWTZ (750,000/=).
7.
Kuimarisha huduma kwa wagonjwa:
Ø Kukabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa Polisi
FFU Ukonga (47,960,000/=)
Ø Kutoa msaada wa fedha za matibabu jumla
shilingi 4,000,000/= kwa watu
mbalimbali hususan wazee na akina mama.
JUMLA KUU 164,272,000/=
No comments:
Post a Comment