Baada
ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na
vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo
yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
- 1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.
- 2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.
- 3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
- 4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.
- 5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.
- 6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:
Kitendo
cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine
CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa
TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo
linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi
ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko
ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.
Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).
Ofisa
wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young
Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye
mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki
ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
VIJANA U15 WAMALIZA ZIARA MOROGORO, SASA KUIVAA BURUNDI
Timu
ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya
miaka 15, imemaliza ziara Morogoro kwa mafanikio baada ya jana Alhamsi
Desemba 8, kuifunga Moro Kids mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa
siku ya jana Ijumaa Desemba 9, mwaka huu timu hiyo ilijifua kwa mazoezi
kwa mujibu wa programu ya Kocha Oscar Mirambo baada ya Morogoro kuleta
timu ya wakubwa tofauti na vijana wenye umri wa chini ya miaka 15.
Hivyo, mchezo huo wa pili haukufanyika.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
Mazoezi
na michezo hiyo ya kirafiki ambayo mingine wataifanya Zanzibar juma
lijalo, ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya
Burundi mchezo unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, mwaka huu kwenye Azam
ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Awali ilipangwa icheze na Shelisheli
ambayo imetoa taarifa ya kuwa haijajiandaa.
Mara
baada ya Morogoro, timu hiyo imerejea Dar es Salaam leo kujiandaa na
safari ya kwenda Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili
mingine ya kirafiki.
Zanzibar
itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016
kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla
ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa
dhidi ya Shelisheli.
Kikosi
hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana weeny umri wa chini
ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa
Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban
Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.
Walinzi
ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid,
Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim
Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.
Viungo
ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula
Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari
Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma Chasambi,
Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.
Timu
hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na
kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza
Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na
sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri
wa miaka miwili hadi sita.
Timu
hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana
mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.
CAPTION
MCHEZAJI
Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, Edson
Mashirakandi akikokota mpira baada ya kumtoka beki Dastan Matheo kwenye
mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
(Picha na Alfred Lucas wa TFF)
KIKOSI
Kikosi
cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yaliyofanyika leo kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
TEACHER
Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, Edson
Mashirakandi (Katikati) akimtoka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oscar Milambo
(Kulia) kwenye mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro. Kushoto ni beki Rashid Hamis (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
WACHEZAJI
Kiungo
Alphonce Mabula (kushoto), akichuana na Jonathan Kombo wakati mazoezi
yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na
Alfred Lucas wa TFF)
……………………………………………………………………………… …………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment