Na: Frank Shija – MAELEZO.
MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni
katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Hayo yamebainishwa na
Katibu wa Chama hicho Jaji C. W. Makuru kupitia taarifa yake kwa vyombo vya
habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imesema
kuwa imesema kuwa Makamu wa Rais
anatarajiwa kuwa mgeni rasm katika Mkutano Mkuu wa nanw wa Chama cha Majaji
Wanawake Tanzania (TAWJA) utakaofanyika kesho (leo) jijini Dar es Salaam.
Imeongeza kuwa mkutano
huo utafanyika katika ukumbi wa PSPF
Goldeni Jubilee Tower ghorofa ya nne na unatarajiwa kuanza majira ya saa moja
na nusu asubuhi kwa wageni waalikwa kuwasili na kujisajili.
Aidha taarifa hiyo
imeongeza kuwa Mkutano huo utatanguliwa na mafunzo ya uandishi wa hukumu na elimu
kuhusu mifuko ya jamii.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na wa wanachama ambao ni Mahakimu na
Majaji 200 kutoka pande zote za Tanzania.
No comments:
Post a Comment