Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya
Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji
Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam
Sports Federation Cup 2017.
Madai
ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu
kwenye Simba dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports
Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Januari 22, mwaka
huu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
KAMBI YA KILIMANJARO WARRIORS
Timu
ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro
Warriors’ inatarajiwa kuingia kambini Janauri 29, 2017 kwa ajili ya
maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali za Olimipiki
zitakazofanyika jijini Tokyo, Japan mwaka 2020.
Kambi
hiyo ya wiki moja itafanyika kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar
es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
No comments:
Post a Comment