KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, January 13, 2017

UAMUZI WA KAMATI YA UTENDAJI YA CAF.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake.

CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


RAIS MALINZI AMPONGEZA MKURUGENZI SINGO 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi amempongeza Bw. Yusuph Singo Omari kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania.

Mapema wiki hii, Yusuph Singo Omari, aliteuliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye kushika wadhifa huo kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Leonard Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.    

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

AZAM SPORTS FEDERATION YAENDELEA

Michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho ya Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), inatarajiwa kuendelea kesho kwa kukutanisha timu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya hatua ya kushirikisha timu za daraja la pili na timu za ligi ya mikoa (RCL) kukamilika.
Kesho Jumamosi Januari 14, mwaka huu, KMC ya Kinondoni itacheza na Kiluvya United ya Pwani kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kabla ya keshokutwa Jumapili Januari 15, mwaka huu kwenye viwanja tofauti.    
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA J’MOSI

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Januari 14, 2017 kwa  michezo miwili.
 Katika michezo hiyo umo wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui FC – zote za Shinyanga ambzo zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage. 
  
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://www.tff.or.tz/news/740-ligi-kuu-ya-vodacom-tanzania-bara-j-mosi

No comments: