Na:
Lilian Lundo – MAELEZO
Washiriki
watatu wa Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika mkoani Ruvuma wanatarajia
kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli nchini Afrika Kusini Februari 19,
2017.
Hayo
yamebainishwa na Muandaaji Mkuu wa Majimaji Selebuka Reinafrida Rwezaura wakati
wa makabidhiano ya tiketi za ndege za kwenda Afrika Kusini kwa washindi hao
yaliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAEELEZO jijini Dar es Salaam.
“Kikubwa
kilichotukutanisha hapa leo ni kuwaaga washindi wa Mbio za Baiskeli katika
tamasha la Majimaji Selebuka 2016, zilizofanyika tarehe 04 Juni 2016 kutoka Mbinga
hadi Songea umbali wa kilomita 100, ambao wanatakiwa kwenda kushiriki
mashindano ya Mbio za Baiskeli Jijini, Johanesburg, Afrika Kusini,” alifafanua
Rwezaura.
Rwezaura
aliwataja washindi hao wanaotegemea kwenda Afrika Kusini kuwa ni Salum Miraji ambaye
alikuwa mshindi wa kwanza , Allen Nyanginywa
ambaye alikuwa mshindi wa pili na Ipyana Mbogela ambaye alikuwa mshindi
wa tatu.
Kwa
upande wake, mshiriki wa mashindano hayo Allen Nyanginywa ameishukuru Taasisi
ya Songea Mississippi (SO-MI) kwa kuandaa mashindano hayo pamoja na kutimiza
ahadi ya kuwasafirisha washindi wa kwanza hadi wa tatu kwenda nchini Afrika Kusini.
Aliendelea
kwa kusema kuwa watahakikisha wanachukua ushindi nchini Afrika Kusini kwani
huko wanaenda kufanya kazi na wamefanya mashindano hayo ya Baiskeli imekuwa ni
kazi yao.
Majimaji
Selebuka ni tamasha linalofanyika kila mwaka mjini Songea, mkoani Ruvuma ambalo
huandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SO-Mi) ambapo kwa mwaka huu 2017 tamasha hilo linatarajia kufanyika
kunzia Julai 23 hadi 30, 2017.
No comments:
Post a Comment