Kikosi cha Bendi ya Matarumbeta ycha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongoza matembezo kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote. |
Umati wa watu pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo |
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiongoza mazoezi ya viungo wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi. |
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwahutubia baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi. |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi. |
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Vijana, Kazi na Ajira), Anthony Mavunde, akiongea jambo akiwa kama Kiongozi mwakilishi wa Mkoa wa Dodoma, mbele ya Viongozi wa Serikali. |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. |
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Na.
Lilian Lundo-Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa ameziagiza
Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi
kufanya mazoezi na kupumzika.
Kassim
Majaliwa ametoa agizo hilo, Mjini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa
Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.
"Ni
muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili,
kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alisema, Majaliwa.
Waziri
Mkuu amesema kwamba, muitikio wa ufanyaji mazoezi wa viungo ni mkubwa, ambapo watu
wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.
Aidha,
amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya
watu kufanya mazoezi na kumpuzika.
Ameongeza
kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya yao na kusiwe na
gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.
Vile
vile amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kuhamasisha mazoezi ya
viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo
ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.
Kwa
upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa
kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya kila mwezi
kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa
yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na saratani.
Naye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba,
mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya Afya pamoja na
TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa vikundi vya mazoezi ya
viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza na watumishi wa Umma.
Aidha
amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo wawahamasishe
wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kulinda afya zao.
Uzinduzi
wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan kuanzia viwanja vya Bunge na baadaye
alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri.
Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge,
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wananchi wa Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment