Ikulu, Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23
Machi, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.
Katika
Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John
Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha,
Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Uteuzi
huu unaanza mara moja.
Wateule
wote wataapishwa kesho Mchana tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu, Jijini Dar es
Salaam.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
23
Machi, 2017
No comments:
Post a Comment