KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, March 24, 2017

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA.

 Mkutano Mkuu wa mwaka wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha, (AICC), leo Machi 23, 2017. Kauli mbiu ya mwaka huu ya mkutano huo ni, "
“Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (pichani juu), ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda..
Waziri ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2017 wakati akifungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa KItuo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
“Nimeelezwa kuwa nyinyi PPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Jeshi la Magereza mmeingia kwenye makubaliano ya pamoja ya kuanzisha viwanda vikubwa na vya kisasa vya kuzalisha sukari katika eneo la Mkulazi na Mbigiri Morogoro.” Alisema Waziri Dkt. Mpango
Akifafanua zaidi kuhusu mpango wa PPF kwa ushirikiano na NSSF na Jeshi la Magereza kwenye uwekezaji mkubwa wa viwanda, Dkt. Mpango alisema, “Mimi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama ni mashuhuda wa hilo kwani tuliweza kujionea eneo la mradi la Mkulazi na ujenzi wa miundombinu tulipolitmbelea katika eneo hilo mwezi Desemba mwaka jana.” Alisema.
Akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw.Ramadhan Khijjah, (pichani juu), alisema, kauli mbiu ya mkutano huu wa 26 wa Wanachama na Wdau wa PPF ni “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Hifadhi ya Jamii”.
“PPF imedhamiria kwa dhati kabisa kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ya kjuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda kama inavyoelezwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/2017 hadi 2010/21.
 Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio alisema Mkutano wa mwaka huu ni wa siku mbili na umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 800 na lengo la kuchagua kauli mbiyo iliyoelezwa hapo juu ya “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii” ili kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.

Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Rmmanuel Martin, akitoa taarifa ya fedha ya Mfuko

No comments: