Na
Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar
es Salaam
7.April,
2017
BODI ya Maziwa
Tanzania imeandaa Mpango Mkakati wa
ushirikiano na Sekta Binafsi ili kuongeza idadi ya ng’ombe wa maziwa kufikia
Milioni 1.5 hatua inayolenga kuongeza wa soko la uzalishaji wa mazao ya maziwa katika
nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini,
Nelson Kilongozi wakati wa mahojiano katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA
kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) na kuratibiwa na
Idara ya Habari (MAELEZO).
Kilongozi
alisema taasisi hiyo imeandaa mkakati huo wa miaka 5 kuanzia mwaka 2018-23 ili
kuhakikisha kuwa viwanda vya Tanzania vinakuwa na uwezo mkubwa wa kusindika
maziwa na kushindana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya katika
uuzaji na usambazaji wa mazao ya maziwa katika ukanda wa Jumuiya hiyo.
“Kwa
sasa Tanzania ina jumla ya Ng’ombe wa maziwa 782,000 kati ya ng’ombe Milioni 28
waliopo, hivyo hawatoshelezi mahitaji yetu, lengo letu ni kushirikiana na sekta
binafsi ili kuhakikisha kuwa tasnia ya maziwa inaleta tija inayokusudiwa”
alisema Kilongozi.
Kwa
mujibu wa Kilongozi alisema uzalishaji wa maziwa nchini kwa sasa ni lita
Bilioni 2.1 kwa mwaka ambapo asilimia 70 yanatokana na ng’ombe wa asili, ambapo
hata hivyo imekuwa ni vigumu kutoa elimu kwa wafugaji wake kutokana na
changamoto ya kuhama mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta malisho.
Aliongeza kuwa kuwa mpaka sasa kuna jumla ya
viwanda 82 vyenye uwezo wa kusindika lita laki 652,000, na hivyo Bodi hivyo
imejipanga katika kuhakikisha kuwa inaongeza hamasa kwa wawekezaji kwa ajili ya
kujenga viwanda vidogo na vya kati ili kulinda ubora wa maziwa ya Tanzania.
“Changamoto
iliyopo sasa ni kukosekana kwa vituo vya ukusanyaji wa maziwa pindi
yanapozalishwa kwa kuwa vituo hivyo havina vifaa vya kupoozea maziwa pindi
yanazalishwa kabla ya kufikishwa kiwandani” alisema Kilongozi.
Alisema
Bodi hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wafugaji kuzingatia kanuni za ufugaji bora
ikiwemo kuwa na mbegu bora zenye uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha cha
maziwa ili waweze kujiongezea kipato sambamba na kuimarisha afya.
Akifafanua
zaidi Kilongozi alisema Bodi hiyo pia imeendelea kuhamasisha wananchi kujenga
tabia ya kunywa maziwa kwa, ambapo kwa mwaka huu wataanzisha Programu maalum ya
uhamasishaji unywaji wa maziwa katika mikoa 6 nchini.
Aliitaja
Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Njombe na Mbeya, ambapo
pamoja na mambo mengine program hiyo imelenga pia kukabiliana na magonjwa ya
udumavu yanayowakabili watoto wadogo katika mikoa mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment