Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akipena mikono na Afisa Elimu, (Taaluma), mkoawa Pwani,Shirley Membi Swai, wakati wa makabidhiano ya mradi wa uwekaji umeme katika shule ya Msingi Galagaza, kata ya Msangeni, Kibaha kwa Mfipamkoani Pwani, Aprili 7, 2017. Mradi huo una thamani ya Shilingi Milioni 10. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Shaaban Langweni.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said.
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi mradi wa umeme kwenye majengo ya
shule ya msingi Galagaza iliyoko, kata ya Msangani wilaya ya Kibaha mkoani
Pwani.
Akikabidhi
mradi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 10, wakati wa hafla fupi
iliyofanyika shuleni hapo Aprili 7, 2017, Meneja wa TANESCO, Mkoani Pwani,
Mhandisi Martin Madulu, alisema “mradi ulihusisha utandazaji nyaya za umeme
(wiring installation), ufungaji wa power
circuit- breaker, taa, pamona na ufundi kwenye majengo yote ya shule ikiwemo
ofisi ya walimu”. Alifafanua meneja huyo.
Akifafanua
zaidi, Mhandisi Madulu alisema, “tumeona tuwaunge mkono shule kwenye level ya
msingi kwani ni maandalizi mazuri kwa wataalamu wa baadaye kwani sasa mazingira
yatakuwa mazuri kwa kusoma, pia mazingira yatakuwa mazuri kwa walimu kuandaa
masomo yao na tunaamini italeta matokeo chanya.” Alisema.
Alisema,
TANESCO imeamua kusaidia shule hiyo katika harakati za shirika kurudisha sehemu
ya faida kwa wananchi, lakini pia kuhamasisha umma kutumia umeme.
“Ni
fursa kwenu kutumia vizuri umeme huu, ili muweze kufanya vizuri zaidi katika
masomo yenu, tunategemea kiwango cha ufaulu kitaongezeka kwani hivi sasa
mnaweza kutumia fursa mbalimbali za kupata elimu kama matumizi ya kompyuta,
ambazo zinahitaji uwepo wa umeme.” Alifafanua.
Akipokea
mradi huo, Afisa Elimu (Taaluma) wa Mkoa wa Pwaniambaye alimwakilisha Afisa
Elimu wa Mkoa huo, Shirley Membi Swai, aliishukuru TANESCO kwa msaada huo na
kuwataka wanafunzi na walimu kutumia vizuri uwepo wa umeme shuleni hapo
kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwani sasa mazingira ya kusoma ni mazuri zaidi.
“
Huu ni mchango mkubwa sana katika maendeleo ya elimu nchini, msaada huu umekuja
kwa muda muafaka kwani hivi sasa, serikali tayari imeanza kufundisha TEHEMA
katika shule na kufundisha kwa kutumia mtandao (digital learning na tayari
umeshaanza hapa nchini, ambapo wanafunzi na walimu wameanza kutumia kompyuta
ndogo (tablets).” Alisema.
Pia
nawashukuru TANESCO kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Dk. John
Magufuli ya kuwapatia wanafunzi elimu bure, msaada huu unaongeza chachu ya
kufanikisha azma hiyo ya serikali.
Mhandisi Martin Madulu, akitoa hotuba yake. |
Afisa Uhusiano wa TANESCO, Salama akizungumza wakati wa utangulizi wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Galagaza.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Galagaza, Shaaban Lagweni, akiwatambulisha walimu wenzake.
Sehemu ya majengo yaliyowekewa umeme na TANESCO kama msaada.
Wanafunzi wakipiga makofi kushangilia hotuba.
Mwalimu Echi Mkopi, akisoma risala.
Kwaya ya shule ikiburudisha.
Mgeni rasmi uongozi wa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananfunzi.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akimuonyesha Afisa Elimu (Taaluma), Shirley Membi Swai,moja ya vifaa vilivyofungwa na TANESCO katika mradi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani waliohudhuria hafla hiyo wakibadilishana mawazo.
No comments:
Post a Comment