Na Tiganya Vincent
6 Mei 2017.
RAS-Tabora.
Serikali
imesema kuwa mwezi Julai mwaka huu (2017)itanunua ndege nyingine mpya
aina ya Dash 8-Q 400 kwa ajili kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania
ili liliweze kutoa kutoa huduma za usafiri wa anga katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi.
Hatua hiyo itaiweza ATCL kufikisha ndege nne (4) ambapo itaiwezesha kuongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na miji ya nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi , Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Kauli
hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano
Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Safiri za Ndege za Shirika
la ATCL mkoani Tabora.
Alisema
kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia Julai mwakani
(2018)Shirika la Ndege hapa nchini linakuwa na uwezo wa kumiliki Ndege
sita zenye uwezo wa kubeba abira kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri
mikoa mingi hapa nchi na nje ya Tanzania.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa hadi hivi sasa , serikali imeshanunua ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
Alisema kuwa hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya Bombardier Dash 8-Q400 ambayo
itakuwa na uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132
kila moja na Boeing 787 (Dreanliner ) itakayokuwa na uwezo wa kubeba
abiria 262.
Aidha
,Mhe. Ngonyani alisema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha inaimarisha viwanja vya
ndege kwa kukarabati miundombinu na kuboresha mifumo mbalimbali ya
huduma za usafiri wa anga.
Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sanjari uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa.
Mhe.
Ngonyani alisema kuwa Serikali kupitia Shirika lake imekusudia
kuhakikisha kuwa mikoa yote hapa nchini inaunganisha na usafiri wa anga.
Alitoa
wito kwa kwa wananchi kutumia usafiri wa anga hasa wa Shirika hilo kama
huduma ya kawaida na ya kuongeza fursa ya kibiashara kwa ajili
kuimarisha kipato kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Mhe.
Ngonyani aliwaomba wakazi wa Tabora na maeneo mengine hapa nchini
kutumia huduma za usafiri wa anga katika kutanua wigo wa biashara zao na
kuhamasisha utalii na kuimarisa sekta ya kilimo cha kisasa hapa nchini.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho alisema kuwa Shirika la Ndege hapa
nchini linatoa huduma nafuu ukilinganisha na mashirika mengine yanayotoa
huduma hiyo hapa nchini.
Alisema
kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia usafiri huo na
kutokuwa wa watu wachache kama yalivyo mashirika mengine hapa nchini.
Dkt.
Chamuriho alisema kuwa Shirika hilo linatoza gharama nafuu
ukilinganisha na Kampuni nyingine zinazotoa huduma za usafiri wa anga
hapa nchini.
Alisema
kuwa hivi sasa kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni
shilingi 330,000/- na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 250,000/-.
Dkt.
Chamuriho aliongeza kuwa safari ya kwenda na kurudi kutoka Dar es
salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 499,000/- na kutoka
Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 380,000/-
Nao
wabunge wa Mkoa wa Tabora na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemshuru Rais Dkt.John Pombe
Magufuli kwa kutimiza ahidi yake kwa vitendo kwa kuanza kiliimarisha
upya Sherika la Ndege hapa nchini.
Waliomba
Serikali kupitia Shirika la ATCL kuendelea kupunza nauli za usafiri wa
ndege ili wananchi wengi waweze kutumia usafiri wa anga hasa kupitia
Shirika lao.
Wamesema kuwa haitakuwa na maana kama nauli zitakuwa juu na wananchi kuona usafiri wa anga ni watu matajiri tu.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wawekeza
popote ndani na nje ya nchi kwenda mkoani humo kuwekeza katika sekta
mbalimbali ikiwemo ya kilimo kufuatia kuimarika kwa miundo mbinu
mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, barabara na mawasiliano ya simu.
Alisema
kuwa Tabora inayoa ardhi nzuri inayokubali ufugaji na ukilima wa mazao
mbalimbali kama vile tumbaku, mahindi, alizeti mbunga, karanga miazi,
mihogo na mengine mengine hatu inayowezo kuwawezesha kufunga viwanda
vidogo na vikubwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya safari za ndege za Shirika hilo mkoani Tabora zitakuwa Jumatau, Jumatano Ijumaa na Jumapili.
No comments:
Post a Comment