KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, May 6, 2017

TAIFA LAPATA MSIBA MKUBWA WA WANAFUNZI ZAIDI YA 26 NA WALIMU WAO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KARATU LEO

Taarifa iliyotufikia katika mtandao huu, inaeleza kuwa kuna ajali imetokea asubuhi leo kuwa  katika eneo la Rhotia Wilaya ya  Karatu Mkoani Manyara, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza muelekeo na kupinduka wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya Karatu. Inadaiwa kuwa wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa. jitihada za kumtafunda Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara zinaendea ili kupata kauli yake juu ya ajali hii. Pichani ni baadhi ya wasamalia wakitoa msaada wa uokozi kwa wanafunzi hao.
Wasamaria wakitoa miili ya waliokufa.
 
Uokoaji ukiendelea.
Gari likiwa katika Bonde.

No comments: