Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru
akizungumza na wauguzi jana mei 19. 2017 katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani
ambayo hufanyika Mei 12, kila mwaka ampapo kitaifa yalitanyika Mkoani Singida hivi karibuni.
Baadhi
ya Mamenena na Wauguzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Museru
Baadhi
ya Wauguzi wauguzi wakiandika jambo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Museru alpokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo.
Wauguzi wakifuatilia jambo wakati maadhimisho hayo
Wauguzi wakiwa katika utulivu wakisikiliza
Wauguzi wakiwa katika utulivu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Museru alpokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo jana mei 19, 2017
Mmoja wa muuguzi akichangia mada katika hayo
Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Sebastian Luziga akizungumza kwenye maadhimisho hayo .
Mweka hazina Msaidizi Tanna Taifa, Josephine Lwambuka (mbele aliyevaa bluu) akisikiliza kwa umakini akiwa na wauguuzi wakati alipokuwa akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam jana Mei 19, 2017
Mkurugenzi wa
Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kulia ) akiwanyesha wauguzi hao kijarida cha shaha ya kitambulisho cha leseni ambacho anahitajika muuguzi kuwanacho ili afanye kazi
Mgeni rami katika Maadhimisho hayo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa akiingia ukumbini
Mkurugenzi
Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru akipokea risala kutoka kwa Debora
Bukuku baada ya kuisoma kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa
Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kulia) akiwaongoza baadhi ya wauguzi kuuwasha mshumaa wakati wa Maadhimisho hayo
Baadhi ya Wauguzi wakiwa wamewasha mishumaa kabla ya kurudi kula kiapa wakati wa Maadhimisho hayo
Mkurugenzi wa
Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa, akiwaongoza Wauguzi kurudi kula kiapo wakati wa Maadhimisho hayo
Baadhi ya Wauguzi wakirudia kiapo kwamba wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uadilifu.
Wauguzi wakirudia kula kiapo wakati wa Maadhimisho hayo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Na Dalila
Sharif.
MKURUGENZI wa
Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa amesema
wauguzi wote wanatakiwa kuwa kitambulisho cha leseni ndio waweze kutoa huduma kwa wateja (wagonjwa) tofauti na hivyo kifungo
cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milion 5.
Akizungumza
Dar es Salaam jana,wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Dunia yaliyofanyika
katika tawi la hospitali hiyo,alisema Agnes kuwa wauguzi wengi hufanya kazi
bila kuwa na vibali vya leseni hali ambayo kinyume na sheria ya hutoaji wa
huduma kwa wagonjwa.
“hivyo
sheria hii itachukua mkondo wake kwa kila muuguzi ambaye ataenda kinyume kwa
kutokuwa na leseni ya utoaji wa huduma
ya pratikali kwa wagonjwa na kuitumikia adhabu hii,”alisema Agnes.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali hiyo,Lawrence Museru alisema kila muuguzi huwa na
kitambulisho cha kufanyia kazi kwa ajili ya kutoa huduma hiyo hivyo kama mtoaji
wa huduma anapaswa kuheshimu taaluma hiyo.
“Hivyo pia
nawataka wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa
katika kutoa maneno yanayostahiki ili kutokuwakwaza kama yanavyosemwa kwa
baadhi ya wafanayakazi kutokuwa na lugha nzuri,”alisema Museru.
Pia
alieeleza kuwa zipo baadhi ya changamoto kwa wafanyakazi kuhusiana na vitendea kazi na
baadhi ya wafanyakazi waliondoka kutokana na kufoji vyeti.
“Hivyo
Hospitali yetu imeweza kupungukiwa na baadhi ya wauguzi walioondoka wenyewe kwa
kutokuwa na vyeti halali hivyo imeweza kupunguza idadi ya wauguzi na kubaki
1200 na kadhalika,”alisema Museru.
Alisema
kukabiliwa na uchache katika chumba cha ICU ambayo inahitaji zaidi waguuzi kwa
ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa hao.
Aliwataka
wauguzi wafanye kazi na kufata maadili ya taaluma kwa kuwa na nidhamu na tabia
njema na kuwabaini wachache wanaochafua taswira ya uuguzi kwa kuwaonya bila
kuwafumbia macho.
“Hivyo
wauguzi mshiriki katika kuongeza mapato ili muweze kuongezewa mapato ya ndani
ambayo itasaidia kulipa baadhi ya madai na kuhusu suala la sare za wauguzi
tunalifanyia kazi kila muuguzi kupatiawa,”alisema Museru.
No comments:
Post a Comment