Uchaguzi
wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), sasa utafanyika Dar es
Salaam badala ya Dodoma na Morogoro - mikoa iliyotangazwa awali.
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, amesema
kwamba taratibu zote zimekamilika na kwamba siku ya uchaguzi ni Jumamosi
Julai 8, mwaka huu.
Wakili
Mushumba ametoa wito kwa wajumbe wote kufika Dar es Salaam Ijumaa Julai
7, mwaka huu kwa ajili ya kufahamu tararibu za awali za uchaguzi.
Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu.
Majina
ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu,
Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande,
Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege.
Nafasi
zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne
wa Kamati ya Utendaji.
FOMU ZA KUWANIA UONGOZI TAFCA
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametoa wito wa walimu wa soka kujitokeza
kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi - ngazi ya taifa.
Mambosasa
ametoa wito huo ikiwa zimebaki siku mbili tu kwa mujibu wa kanuni
kukamilisha hatua hiyo. Fomu hizo zinazopatikana ofisi ya Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, zilianza kutolewa juzi Julai 3,
2017 na mwisho ni Julai 7, mwaka huu.
“Wanaojitokeza
wachache. Wengine wanadai hawafahamu zilizo ofisi za DRFA. Tunatoa wito
wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali,” amesema Mambosasa.
Nafasi
zilizotangazwa kuwaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,
Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000
wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.
UCHAGUZI CHAMA CHA WATAALAMU WA TIBA ZA MICHEZO
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo
(TASMA), kimetangaza Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kwamba utafanyika
Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es
Salaam.
“Wanachama
wote wanakaribishwa kushiriki kwa namna moja au nyingine katika zoezi
hili muhimu sana,” amesema Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda
alipokuwa anatangaza ramani ya mchakato wa uchaguzi huo leo Alhamis
Julai 06, 2017.
Amesema:
Mwanachama ye yote anayependa kukiongoza chama hiki anaombwa kuchukua
fomu katika ofisi za Olimpiki Maalumu, zilizoko jirani na Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kugombea nafasi anayoona kuwa anaweza
kuimudu.”
Nafasi
zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati
nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji
fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.
……………………………………………………………………………… …….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment