Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), inatarajiwa kuketi kwa siku mbili Agosti 20 na 21, 2017
kupitisha usajili, lakini kabla kupitisha itasikiliza malalamiko kutoka
baadhi ya timu na vituo vya kuibua na kukuza vipaji vya soka zinazodai
fidia baada ya wachezaji wao kusajiliwa na klabu nyingine msimu wa
2017/18.
Viongozi
au Wawakilishi wa Klabu zifuatazo hawana budi kufika Azam FC, Pamba FC,
African Lyon, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Singida United, Tusker FC,
Young Africans, Njombe Mji, Majimaji, KMC, Ndanda FC, Coastal Union,
Stand United, Rhino FC, Mbao FC, Toto Africans, Stand United, Mbeya City
na Lipuli. Pia wameitwa wachezaji Mbaraka Yussuf na Frank Hamisi.
Klabu
na vituo vya kuibua na kukuza vipaji vilileta malalamiko yao TFF kudai
fidia mbalimbali kama vile za mafunzo; ada ya usajili; ada za maendeleo
na kuvunjwa kwa mikataba kutoka katika timu walizochezea hadi msimu
uliopita.
Baadhi
ya malalamiko yaliyopokelwa TFF ni ya Majimaji ya Songea dhidi ya Azam
FC ya Dar es Salaam kuhusu mchezaji Idd Kipangwile.
Alliance
ya Mwanza imelalamikia Pamba pia ya Mwanza kuhusu mchezaji Juma Nyangi
ambako madai hayo yamekwenda mbali zaidi yakisema kuwa mchezaji husika
amebadili jina kwa lengo la kudanganya.
Kwa
upande wake, African Lyon imeondokewa na wachezaji 19 na inadai fidia
katika timu, wachezaji kwenye mabano za Majimaji (Saleh Malande); Lipuli
(Hamad Manzi, Lambele Reuben na Mussa Nampoka); Young Africans (Rostand
Youthe Jehu); Tusker FC (Abdul Hilal) na Ndanda kwa wachezaji Hamad
Tajiri na Baraka Majogoo.
Madai
mengine ni dhidi ya Coastal Union kwa wachezaji Baraka Jaffary, Omary
Salum, Raizen Hafidh na Fred Lewis huku madai mengine ni kwa Kagera
Sugar kwa wachezaji Omar Abdallah, Abdallah Mguhi na Vicent Ludovic na
Alhaji Zege .
Madai
mengine ni dhidi ya timu ya Kinondoni Municipality Council (KMC) ambayo
imewasajili Halfan Twenye, Yussuf Abdul na Rehani Kibingu wakati
Singida United inalalamikiwa kumsajili Miraji Adam ilihali Njombe Mji
inadaiwa fidia kwa kumsajili mchezaji Salum Juma.
Malalamiko
mengine ni ya Kisa Academy ya Kinondoni, Dar es Salaam dhidi ya timu za
Mbeya City (Idd Seleman); Majimaji (Jafar Mohammed); Mbao (Ally
Rashid); Stand United (Said Mbati) na Friends Rangers (Hassan Abubakar).
Madai
mengine dhidi ya timu za Coastal Union (Abubakar Nyakarungi na Ahmed
George); The Mighty Elephant (Maliki Hamad); Kagera Sugar (Hussein Idd)
na Azam FC (Omary Maunda).
…………………….……………………………………………………… …………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment