Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk, Harrison Mwakyembe akizungumza katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dodoma.
![]() |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk, Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem mara walipokutana katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dodoma.![]() Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk, Harrison Mwakyembe (katikati walio kaa) katika pich ya pamoja na maafisa mbalimbali wa serikali, kuanzia kushoto waliokaa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem. |
Na Mwandishi Wetu
Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al-Najem ameshiriki katika Kongamano la Kimataifa la Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki CHAKAMA ambalo limefanyika siku mbili katika mji mkuu Dodoma, kongamano hilo lilihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk, Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Dk, Suzan Kolimba ambao walitoa shukrani zao kwa Ubalozi wa Kuwait kutokana na mchango wake katika kufadhili baadhi ya gharama za kongamano hilo baada ya kupokea ombi kutoka wizara ya Nje.Balozi Al-Najem alitoa hotuba katika kongamano hilo ambapo alieleza kuwa swala la kubadilisha biashara na utamaduni baina ya nchi za Ghuba na mataifa ya Afrika Mashariki lilikuwepo tangu mwanzoni mwa karne ya ishirini, bandari za Dar es salaam, Zanzibar, na Mombasa zilikuwa kimbilio la wafanyabiashara, na kwa sifa ya kipekee meli za Kuwait zilikuwa zikitia nanga katika bandari hizo na tunaweza kusema kuwa hakuna nyumba ya Kikuwait ilikuwa inakosa nguzo za ujenzi ambazo zilikuwa zinaletwa kutoka Afrika Mashariki.
Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki CHAKAMA kilichoanzishwa mwaka 2002 kiliandaa kongamano hilo ambalo pia lilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Zanzibar, Kenya, Uganda, Ghana na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment